Sale!

$15.00

Hazina YA Ushairi, David Coniam, 9789966181886

Author: David Coniam
SKU: 9789966181886 Category: Tag: Product ID: 146644

Description

Hazina ya Ushairi ni kazi ambayo inadhamiria kuondoa ugumu wa uchambuzi wa mashairi na kuufanya uwe somo linalowezekana kusomwa, kufurahiwa na kuchambuliwa na mwanafunzi pasipo kumhitaji sana mwalimu wake. Ukiwadadisi wanafunzi maoni yao kuhusu somo la ushairi utagundua kuwa asilimia kubwa sana wasingalipenda litahiniwe.Kisa na maana ni kwamba linachukuliwa kuwa somo la kuogofya na walimu wengi, falaula mwanafunzi aliyezongwa na masomo mengine mengi ‘magumu’! Wengi hawaoni sababu ya kusumbuliwa na mashairi hasa ikikumbukwa kwamba ujuzi wake hauhitajiki mtu anaposaka gange. Mwelekeo huu hasi ni tisho kubwa linaloelekea kuangamiza fahari na umuhimu wa ushairi miongoni mwa vizazi vichanga. Wataalamu wa awali walitunga diwani na wenzao kuzichambua.Wengi wa hao waliozichambua walisahau kutoa ushairi mikononi mwa Mswahili. Waliishia kuutwaa vile ulivyokuwa katika enzi za Muyaka bin Haji na kumkabidhi mwanafunzi asiyehusiana naye kwa lolote wala chochote kisha wakamtaka aipende na kuionea fahari fasihi ya Kiswahili kama alivyopenda Mwalimu Simtaji na wengineo. Matokeo yake ni kwamba taabu za mwanafunzi hazikufikiriwa katika diwani zile wala katika tahakiki zao. Aidha, istilahi za ushairi, hasa zenye asili ya Kiarabu, zilimkaba koo, msamiati wa kishairi [lugha za kilahaja] ulimzonga pumzi, na arudhi kadha zikamtisha na kumtamausha akawa mnyonge kweli. Kwa sababu hiyo, hata kazi sahili na wa kupendeza zisizohitaji tafakuri, kama vile mashairi ya Kwa wanafunzi wa shule za upili vii watunzi wa kileo kama Alamin Mazrui, Said Ahmed Mohamed, Fikeni Sonkoro, David Massamba, Mugyabuso Mulokozi, Kithaka wa Mberia na wengine wengi, hazipati umaarufu unaostahiki miongoni mwa vijana. Diwani zilizosomwa na walimu na wanagenzi wao zilikuwa zizo hizo zinazowanyima raha wanafunzi darasani. Matokeo ni kuwa vyuo vilizaa walimu wengi wasioyapenda mashairi na vitabu visivyoeleweka viliwanyima starehe. Nao waliingia navyo madarasani; kufunza ati! Walipomaliza kufunza wanafunzi walitamani sana somo hilo liondolewe kabisa kwenye silibasi. Hivyo basi mimi situngi diwani, nahifadhi hazina ya ushairi; kumbukumbu ya kurejelewa na mwalimu na mwanafunzi darasani.

Additional information

ISBN

Page Number

Author

Publisher